Swahili

[vc_row css_animation=”” row_type=”row” use_row_as_full_screen_section=”no” type=”full_width” angled_section=”no” text_align=”left” background_image_as_pattern=”without_pattern”][vc_column width=”1/4″][/vc_column][vc_column width=”3/4″][vc_column_text]MAELEZO KUTOKA KATIKA WAEBRANIA 9:27,28.

UHAKIKISHO NNE KUBWA NI,
1) KIFO
2)HUKUMU
3)KIFO CHA BWANA YESU
4)KURUDI KWA BWANA YESU MARA YA PILI.

Ulimwengu umejawa na ukosefu wa
haki. Hatuna huakika kamwe. Mafuriko,moto,tetemeko la
ardhi yote yanaaribu na kuangamiza mijini na  ulimwengu  wote.
Majambazi wauwa  wat na kuaribu vitu
vyetu,familia na hata marafiki wetu. Runinga huleta habari ya vita, watu wengi
waachishwa kazi,wengi wapoteza makao, maiaha na biashara.
Tuaminio watuvunja mioyo. Kila mmja ajaribu kutafuta haki na
mahali pa kuweka tumaini.
Kwenye huu ulimwengu usio na matumaini, tuna uhakika
nne ambayo hatutaweza puuuza kamwe:

1. KIFO

 

Ni hakika mwnadamu atakufa. Siku wala saa haijulikani lakini ni
hakika tutakufa, hatuta chelewa wala kuendeleza siku ya kufa kwetu kama vile
watu wanavyo wekwa kufa mara moja. Wengine watakufa wakiwa wadogo bado na wengineo katika umri wa 80 ama 90 lakini wote watakufa.
Wanasayansi na miujiza yao, madawa ya bei ghali na
mahosipitali ya kifahari wote hawawezi kamwe zuia kifo. ”
Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakaporudi ardhi ambayo katika
hiyo ulitwaliwa kwa maana u mavumbi we we nawe mavumbini utarudi” Mwanzo
3:19)
Adamu alipo tenda dhambi, yeye na wanawe wote walilaaniwa kufa kwa hivyo sisi
sote tunakufa sababu sisi sote ni wana wa Adamu. Na
sote
  tu wenye dhambi.Makosa ya Baby wetu Adamu iliwekwa kwetu.
Sote tumepungukiwa.  Mwili huu tunao lazina ife.
Mfalme Daudi alikubaliana na neno hili aloposema, ” Mwanadamu siku zake zi
kama manani, kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo, mamana upepo hupita juu yake  kumbe haliko! Na mahali pake hapatalijua tena”.
(Zaburi 103:15,16) Ayubu naye akasema,” Mmoja
hufa katika nguvu zake kamili, mwenye kukaa salama na kustarehe; mwingine hufa
katika uchungu wa roho, asionje mema kamwe”. (Ayubu 21:23,25).


2. HUKUMU.

Wengi hawajali kufa, wao hufikiria kifo ndiyo mwisho wao. Kifo ni mwanzo wa uzima wa milele, maisha inayojaa furaha kwa
wale wakufao kwa Bwana Yesu au maisha ya uzuni kwa wale wasio amini Yesu.
Hatuwezi kamwe puuza hukumu tuna hakika kukutana na
hakimu wetu Bwana Yesu kama mhukumu wetu.
Mungu mwenyewe ameteuwa siku ya kuhukumu dunia yote. Kila mtu, mwanamme,
mwanamke na watoto wote watasimama mbele ya Mungu
kuhukumiwa. Mtume Paulo hatuonya hivi,” Lakini wewe je! Mbona wamhukumu
ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? , kwa maana sisi sote
tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu , kwa
kuwa imeandikwa , kama niishivyo , anena Bwana kila goti litapigwa mbele zangu
, na kila ulimi utamkiri Mungu. Basi hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa
habari zake mwenyewe mbele za Mungu”( Warumi
14:10_12). Paulo tena atwambia ” Kwa maana imetupasa sisi sote
kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya
mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda kwamba ni mema au  mabaya“( 2Wakorintho 5:10).
Basi macadamia, kila neno lisilo maana, watakalolinena,wanadam
watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa
haki, na kwa maneno yako utahukumiwa”( Mathayo 12:36,37). Kila mmoja
atahukumiwa kadiri ya matendo yake, ” Atakaye lipa kila mtu kadiri ya
matendo yake”( Warumi 2:6).
Mungu ajua yote na kila tendo
kitawekwa wazi mbele zake bila kupuuza hata tendo moja. Uwe tajiri, masikini , Muheshimiwa, wasomi,weusi ,wekundu na weupe kila
mtu atahukumiwa bila ubaguzi. Mhukumu wetu ni wa haki
na kweli.  ” Basi msiogope, kwa maana hukumu
neno lililositarika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichuliwa, ambalo
halitajulikana”( Mathayo 10:26).  
Maana
mtu awaye yote atakaye shika sheria yote akajikwaa katika neno
moja amekosa juu ya yote” ( Yakobo 2:10).  “Kwa maana sisi sote
tumekuwa kama mtu aliye mchafu na matendo yetu yetu yote ya haki yamekuwa kama
nguo iliyotiwa unajisi, sisi sote twanyauka kama jani na maovu yetu yatuondoa
kama upepo uondoavyo”  (Isaya
64:6).   Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini
mwiahowe ni njia za mauti”( Methali
14:2).   Na mataifa yote yatakusanyika mbele zake ,
Naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi na hao watakwenda
zao kuingia katika adhabu ya milele bali wenye haki watakwenda katika uzima wa
milele” (Mathayo 25:32).

 


3) KIFO CHA YESU.

Yesu alikufa kwa ajili ya kuokoa rafiki zake.
“Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa
ajili ya rafiki zake” ( Yohana 15:13). Binadamu
hangeweza jiokoa mwenyewe. Sote tu wenye dhambi mbele ya Mungu na tunastahili kufa. Time Paulo atuambia ” Kwa sababu
wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa
Mungu (Warumi 3:23).  Kwa maana mshahara ya dhambi ni
mauti bali karamu ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana
Wetu” (Warumi 6:23). Mungu arehemu anaowapenda kama
vile Mtume Paulo atuelezea ” Kwa maana hapo tulopokuwa hatuna nguvu,
wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya maovu; kwa kuwa ni shida mtu
kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki lakini yawezekana mtu kudhubutu kufa kwa
ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu
sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye
dhambi” (  Warumi 5:6,7,8).  Yesu ni Mungu. Muumbaji wa mbingu na
nchi yote. Alilipa deni yetu miaka 2000 iliyopita. Alitolewa sadaka mara moja.
Kifo chake ni hakikiasho kwamba wanao mwamini wako
salama. Wanaokolewa toka kwa dhambi wakihesabiwa haki
na wataololewa siku ya mwisho. Mtume Paulo atuambia
Kwa
kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu kwa Bwana
wetu Yesu Kristo ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba
twakesha au kwamba tea lala” (1Wathesalonika 5:9,10). Kwa sababu wamefanya
dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”
(Warumi 3:24).  Waaminio Bwana Yesu watakuwa na
raha milele. Ni maana gani kuamini Yesu?. Yamaanisha
kumkubali yesu kama Mwokozi na kuelewa maneno yake
kwenye Bibilia takatifu. Maneno yake ni kweli kabisa.
Yesu ni Mungu na tena binadamu, alikufa kwa ajili ya dhambi zetu
,akafufuka
tena baada ya siku tatu na hakika yu hai. Wanwaminio
wamehesabiwa haki sio kwa haki yao , ila  kwa matendo yao bali kwa sababu
Bwana Yesu alikufa kwa ajili ya wenye dhambi. Sote tu wenye dhambi na hatuwezi
amini neno la Bwana kwa nguvu zetu ama akili yetu bali kwa neema yake Yesu
Kristo ” Kwa maana mnaokolewa kwa neema kwa njia ya imanu ambayo hiyo
haikutokana   na nafsi zenu ni kipawa cha Mungu, wala si  kwa
matendo, mtu awe yote asije akajisifu” (Waefeso 2:8,9).  ” Basi ndugu zangu nawaarifu ile injili niliyowahubiri
ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnaokolewa ikiwa mnayashika sana
maneno niliyo wahubiri isipokuwa mliamini bure kwa maana naliwatolea ninyi hapo
mwanzo yake iliyoyapokea mimi mwenyewe ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya
dhambi zetu kama yanenayo maandiko” (1 Wakorintho 15:1_4).  Sass basi
hakuna hukumu ya dhambi juu yao walio katika Kristo
Yesu” (Warumi 8:1). Umeokolewa law ajili ya kifo cha Yesu Kristo msalabani
mlimani Kalvari miaka 2000 iliyopita. Kwa wale wamngojea Kristo Yesu, , Yesu atakuja mara ya pili sio kwa dhambi bali kwa
ukombozi yetu.

4)  YESU KRISTO ATARUDI

MARA YA PILI.

Imepita miaka tangu atoke duniani, Wengi hucheka na
kupuuza ukweli wa kuja kwake Kristo mara ya Hakika Yesu akuja tena. Kwa wale
wamngojea kwa imani,  atakuja kuwaokoa. ” Sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja
na malaika na Sauti ya Malaika mkuu na parapanda ya Mungu, nao walio kufa
katika Kristo, watafufuliwa kwanza, kisha sisi tulio hai tuliosalia,
tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani na hivyo
tutakuwa na Bwana milele” (1Wathesalonika 4:16,17) na ole wao wanao mcheka
Yesu Kriso ” na kuwalipa  ninyi mteswao raha  pamoja na sisi,
wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu  kutoka mbinguni pamoja na malaika
ya uweza wake. Katika mwili wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua
Mungu na wao wasiotii injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi
ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake”(  2
Wathesalonika 1:7,8,9).


HAKIKISHO NNE KUBWA

1) UTAKUFA
2)UTAFIKA MBELE YA HAKIMU KUHUKUMIWA KWA DHIDI YA
MATENDO YAKO.
3)BWANA YESU ALIJITOLEA KUFA MARA MOJA KWA DHAMBI
ZETU.
4) BWANA YESU KRISTO YU HAI NA ATAKUJA MARA YA PULI DUNIANI .
Ukikubali kwamba wewe ni mwenye dhambi na umeenda
kinyume na maagizo ya Mungu, yafaa ufikirie sana maisha yajayo. Hakuna njia
yoyote ila kumkubali Kristo Yesu. Omba Mungu akuregemu
akurehemu, akusamehe dhambi zako akupe neema na rehema
umkubali Bwana yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za watu wake, na baada ya siku
tatu akafufuka na hakika atarudi Ulimwengu kuwaokowa wamwaminiye. Wale
wanaimngojea Bwana Yesu kwa imani wataishi milele mbinguni ”  Na
kifo, uzuni, kilio, naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti
haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena;
kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Wala hapata kuwa na usiku tena;
wala hawana hajaa ya taa wala ya nuru au jua kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru
nao watatawala hata milele na milele”  (Ufunuo
21:4 Ufunuo 22:5).
AMEN AMEN!!!.[/vc_column_text][/vc_column][/vc_row]