Present Truth 

UHAKIKA NNE KUBWA.

Je, unaweza kuwa na uhakika juu ya jambo lolote ?

 

MAELEZO KUTOKA KATIKA WAEBRANIA 9:27,28.

UHAKIKISHO NNE KUBWA NI,
1) KIFO
2)HUKUMU
3)KIFO CHA BWANA YESU
4)KURUDI KWA BWANA YESU MARA YA PILI.


    Ulimwengu umejawa na ukosefu wa haki. Hatuna huakika kamwe. Mafuriko,moto,tetemeko la ardhi yote yanaaribu na kuangamiza mijini na  ulimwengu  wote. Majambazi wauwa  wat na kuaribu vitu vyetu,familia na hata marafiki wetu. Runinga huleta habari ya vita, watu wengi waachishwa kazi,wengi wapoteza makao, maiaha na biashara. Tuaminio watuvunja mioyo. Kila mmja ajaribu kutafuta haki na mahali pa kuweka tumaini.
Kwenye huu ulimwengu usio na matumaini, tuna uhakika nne ambayo hatutaweza puuuza kamwe:


                   1. KIFO


Ni hakika mwnadamu atakufa. Siku wala saa haijulikani lakini ni hakika tutakufa, hatuta chelewa wala kuendeleza siku ya kufa kwetu kama vile watu wanavyo wekwa kufa mara moja. Wengine watakufa wakiwa wadogo bado na wengineo katika umri wa 80 ama 90 lakini wote watakufa. Wanasayansi na miujiza yao, madawa ya bei ghali na mahosipitali ya kifahari wote hawawezi kamwe zuia kifo. "
Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakaporudi ardhi ambayo katika hiyo ulitwaliwa kwa maana u mavumbi we we nawe mavumbini utarudi" Mwanzo 3:19)
Adamu alipo tenda dhambi, yeye na wanawe wote walilaaniwa kufa kwa hivyo sisi sote tunakufa sababu sisi sote ni wana wa Adamu. Na  sote  tu wenye dhambi.Makosa ya Baby wetu Adamu iliwekwa kwetu. Sote tumepungukiwa.  Mwili huu tunao lazina ife. Mfalme Daudi alikubaliana na neno hili aloposema, " Mwanadamu siku zake zi kama manani, kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo, mamana upepo hupita juu yake  kumbe haliko! Na mahali pake hapatalijua tena". (Zaburi 103:15,16) Ayubu naye akasema," Mmoja hufa katika nguvu zake kamili, mwenye kukaa salama na kustarehe; mwingine hufa katika uchungu wa roho, asionje mema kamwe". (Ayubu 21:23,25).
         


                2. HUKUMU.


Wengi hawajali kufa, wao hufikiria kifo ndiyo mwisho wao. Kifo ni mwanzo wa uzima wa milele, maisha inayojaa furaha kwa wale wakufao kwa Bwana Yesu au maisha ya uzuni kwa wale wasio amini Yesu. Hatuwezi kamwe puuza hukumu tuna hakika kukutana na hakimu wetu Bwana Yesu kama mhukumu wetu.
  Mungu mwenyewe ameteuwa siku ya kuhukumu dunia yote. Kila mtu, mwanamme, mwanamke na watoto wote watasimama mbele ya Mungu kuhukumiwa. Mtume Paulo hatuonya hivi," Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? , kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu , kwa kuwa imeandikwa , kama niishivyo , anena Bwana kila goti litapigwa mbele zangu , na kila ulimi utamkiri Mungu. Basi hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu"( Warumi 14:10_12). Paulo tena atwambia " Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda kwamba ni mema au  mabaya"( 2Wakorintho 5:10).
Basi macadamia, kila neno lisilo maana, watakalolinena,wanadam watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa"( Mathayo 12:36,37). Kila mmoja atahukumiwa kadiri ya matendo yake, " Atakaye lipa kila mtu kadiri ya matendo yake"( Warumi 2:6).
    Mungu ajua yote na kila tendo kitawekwa wazi mbele zake bila kupuuza hata tendo moja. Uwe tajiri, masikini , Muheshimiwa, wasomi,weusi ,wekundu na weupe kila mtu atahukumiwa bila ubaguzi. Mhukumu wetu ni wa haki na kweli.  " Basi msiogope, kwa maana hukumu neno lililositarika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichuliwa, ambalo halitajulikana"( Mathayo 10:26).   " Maana mtu awaye yote atakaye shika sheria yote akajikwaa katika neno moja amekosa juu ya yote" ( Yakobo 2:10).  "Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu na matendo yetu yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi, sisi sote twanyauka kama jani na maovu yetu yatuondoa kama upepo uondoavyo"  (Isaya 64:6).   Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwiahowe ni njia za mauti"( Methali 14:2).   Na mataifa yote yatakusanyika mbele zake , Naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele" (Mathayo 25:32).

 

            3) KIFO CHA YESU.


Yesu alikufa kwa ajili ya kuokoa rafiki zake. "Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake" ( Yohana 15:13). Binadamu hangeweza jiokoa mwenyewe. Sote tu wenye dhambi mbele ya Mungu na tunastahili kufa. Time Paulo atuambia " Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Warumi 3:23).  Kwa maana mshahara ya dhambi ni mauti bali karamu ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana Wetu" (Warumi 6:23). Mungu arehemu anaowapenda kama vile Mtume Paulo atuelezea " Kwa maana hapo tulopokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya maovu; kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki lakini yawezekana mtu kudhubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi" (  Warumi 5:6,7,8).  Yesu ni Mungu. Muumbaji wa mbingu na nchi yote. Alilipa deni yetu miaka 2000 iliyopita. Alitolewa sadaka mara moja. Kifo chake ni hakikiasho kwamba wanao mwamini wako salama. Wanaokolewa toka kwa dhambi wakihesabiwa haki na wataololewa siku ya mwisho. Mtume Paulo atuambia " Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba tea lala" (1Wathesalonika 5:9,10). Kwa sababu wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:24).  Waaminio Bwana Yesu watakuwa na raha milele. Ni maana gani kuamini Yesu?. Yamaanisha kumkubali yesu kama Mwokozi na kuelewa maneno yake kwenye Bibilia takatifu. Maneno yake ni kweli kabisa. Yesu ni Mungu na tena binadamu, alikufa kwa ajili ya dhambi zetu ,akafufuka tena baada ya siku tatu na hakika yu hai. Wanwaminio wamehesabiwa haki sio kwa haki yao , ila  kwa matendo yao bali kwa sababu Bwana Yesu alikufa kwa ajili ya wenye dhambi. Sote tu wenye dhambi na hatuwezi amini neno la Bwana kwa nguvu zetu ama akili yetu bali kwa neema yake Yesu Kristo " Kwa maana mnaokolewa kwa neema kwa njia ya imanu ambayo hiyo haikutokana   na nafsi zenu ni kipawa cha Mungu, wala si  kwa matendo, mtu awe yote asije akajisifu" (Waefeso 2:8,9).  " Basi ndugu zangu nawaarifu ile injili niliyowahubiri ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnaokolewa ikiwa mnayashika sana maneno niliyo wahubiri isipokuwa mliamini bure kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yake iliyoyapokea mimi mwenyewe ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kama yanenayo maandiko" (1 Wakorintho 15:1_4).  Sass basi hakuna hukumu ya dhambi juu yao walio katika Kristo Yesu" (Warumi 8:1). Umeokolewa law ajili ya kifo cha Yesu Kristo msalabani mlimani Kalvari miaka 2000 iliyopita. Kwa wale wamngojea Kristo Yesu, , Yesu atakuja mara ya pili sio kwa dhambi bali kwa ukombozi yetu.
           


              4)  YESU KRISTO ATARUDI
                    MARA YA PILI.


Imepita miaka tangu atoke duniani, Wengi hucheka na kupuuza ukweli wa kuja kwake Kristo mara ya Hakika Yesu akuja tena. Kwa wale wamngojea kwa imani,  atakuja kuwaokoa. " Sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na malaika na Sauti ya Malaika mkuu na parapanda ya Mungu, nao walio kufa katika Kristo, watafufuliwa kwanza, kisha sisi tulio hai tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa na Bwana milele" (1Wathesalonika 4:16,17) na ole wao wanao mcheka Yesu Kriso " na kuwalipa  ninyi mteswao raha  pamoja na sisi, wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu  kutoka mbinguni pamoja na malaika ya uweza wake. Katika mwili wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu na wao wasiotii injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake"(  2 Wathesalonika 1:7,8,9).


     
          HAKIKISHO NNE KUBWA


1) UTAKUFA
2)UTAFIKA MBELE YA HAKIMU KUHUKUMIWA KWA DHIDI YA MATENDO YAKO.
3)BWANA YESU ALIJITOLEA KUFA MARA MOJA KWA DHAMBI ZETU.
4) BWANA YESU KRISTO YU HAI NA ATAKUJA MARA YA PULI DUNIANI .
Ukikubali kwamba wewe ni mwenye dhambi na umeenda kinyume na maagizo ya Mungu, yafaa ufikirie sana maisha yajayo. Hakuna njia yoyote ila kumkubali Kristo Yesu. Omba Mungu akuregemu akurehemu, akusamehe dhambi zako akupe neema na rehema umkubali Bwana yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za watu wake, na baada ya siku tatu akafufuka na hakika atarudi Ulimwengu kuwaokowa wamwaminiye. Wale wanaimngojea Bwana Yesu kwa imani wataishi milele mbinguni "  Na kifo, uzuni, kilio, naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Wala hapata kuwa na usiku tena; wala hawana hajaa ya taa wala ya nuru au jua kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru nao watatawala hata milele na milele"  (Ufunuo 21:4 Ufunuo 22:5).
      AMEN AMEN!!!.

 Top
Front Page
Share this Site
with a Friend
Print